Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Machi 12, 2026 Local time: 18:23

Wafanyakazi wa zimamoto Uturuki wamedhibiti mioto mikubwa ya msituni

Mfano wa moto mkubwa uliozuka katika misitu miwili mikubwa nchini Uturuki
Mfano wa moto mkubwa uliozuka katika misitu miwili mikubwa nchini Uturuki

Mioto hiyo katika jimbo la pwani la Izmir magharibi mwa Uturuki na jimbo la kaskazini la Bolu

Wafanyakazi wa zima moto nchini Uturuki wamedhibiti mioto miwili mikubwa ya msituni ambayo ilikuwa inawaka kwa siku tatu, huku mioto mingine ya porini ikitarajiwa kuzimwa hivi karibuni, Waziri wa Misitu alisema Jumapili.

Mioto hiyo katika jimbo la pwani la Izmir magharibi mwa Uturuki na jimbo la kaskazini la Bolu uiianza Alhamisi usiku na wafanyakazi wa zima moto tangu wakati huo wamekuwa na kazi ya kuudhibiti moto huo.

Akizungumza katika wilaya ya Karsiyaka huko Izmir, Waziri wa Misitu Ibrahim Yumakli alisema juhudi za kupunguza nguvu ya moto zinaendelea ili kuzima kabisa moto huo. Moto mdogo uliozuka katika wilaya ya Urla huko Izmir siku ya Jumamosi pia ulidhibitiwa, alisema.

Forum

XS
SM
MD
LG