Vyombo vy ahabari vya Afrika kusini vimetaja mgomo huo kuwa wa kwanza mkubwa kuwahi kufanywa na wafanyakazi wa serikali kwa muda wa mwongo mzima.
Mgomo huo unatarajiwa kusababisha usumbufu katika utoaji wa huduma katika ofisi za serikali na katika viwanja vya ndege.
Wanachama wa muungano wa wafanyakazi wa serikali PSA, wamekuwa wakifanya mgomo wakati wa saa za chakula cha mchana, lakini mgomo huo sasa unaonekana kuongezeka na kupelekea ofisi kufungwa katika miji mikubwa kote Afrika kusini.
Mazungumzo kati ya serikali na waakilishi wa muungano wa wafanyakazi yamekosa kufanikiwa. Wafanyakazi wanataka nyongeza ua mshahara ya asilimia 6, huku serikali ikishikilia kwamba inaweza kutekeleza nyomgeza ya asilimia 3 pekee.