Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Mei 27, 2024 Local time: 12:54

Wafanyakazi wa ICRC waliotekwa nyara nchini Congo wameachiliwa


Nembo ya kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC)
Nembo ya kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC)

Kamati ya kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) ilisema mwishoni mwa mwezi Novemba kuwa raia mmoja wa Congo na mfanyakazi wa kimataifa walitekwa nyara katika jimbo la Kivu kaskazini mahala ambako darzeni ya wanamgambo wenye silaha wanaendesha harakati zao

Wafanyakazi wawili wa Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu (ICRC) waliotekwa nyara mwezi uliopita huko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo wameachiliwa, shirika hilo la kibinadamu limesema Jumamosi.

ICRC ilisema mwishoni mwa mwezi Novemba kuwa raia mmoja wa Congo, na mfanyakazi wa kimataifa walitekwa nyara katika jimbo la Kivu kaskazini, mahala ambako darzeni ya wanamgambo wenye silaha wanaendesha harakati zao.

Mfano wa gari zinazotoa huduma za ICRC
Mfano wa gari zinazotoa huduma za ICRC

"Tumefarijika kurejea kwa wenzetu na tunafurahi kwamba wamefanikiwa kurejea kwenye familia zao, Rachel Bernhard, mkuu wa ujumbe wa ICRC nchini Congo, aliliambia shirika la habari la Reuters. Tungependa kusisitiza kwamba huu utekaji nyara na mashambulizi mengine yote dhidi ya wafanyakazi wa misaada, yanaweza kuhatarisha shughuli zinazofanywa kuzisaidia jamii zilizoathiriwa sana na mzozo". Hakutoa maelezo zaidi kuhusu utekaji nyara au kuachiliwa kwao.

Umoja wa Mataifa na mashirika ya kibinadamu yameonya kuhusu ongezeko la mashambulizi dhidi ya wafanyakazi wanaotoa misaada huko mashariki mwa Congo. Wafanyakazi watatu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi walijeruhiwa siku ya Jumatano huko Kivu kaskazini, wakati gari lao liliposhambuliwa.

XS
SM
MD
LG