Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Septemba 14, 2024 Local time: 03:55

Wafanyakazi Nigeria wamezima mitambo ya umeme wakitaka malipo


Rais wa Nigeria Bola Tinubu. June 23, 2023
Rais wa Nigeria Bola Tinubu. June 23, 2023

Kampuni ya kuzalisha umeme nchini Nigeria imesema kwamba mitambo yako imezima baada ya wafanyakazi kuanza mgomo.

Muungano mkubwa wa vyama vya wafanyakazi nchini Nigeria ilitangaza mgomo kuanzia leo Jumatatu, baada ya kushindwa kukubaliana na serikali kuhusu kiwango cha chini cha malipo kinachostahili kutolewa kwa wafanyakazi.

Nigeria labour congress NLC na Trade union congress TUC vilitangaza mnamo Mei tarehe 1 kwamba wanachama wake wataanza mgomo iwapo makubaliano kuhusu kiwango cha chini cha mshahara yatakuwa hayajafikiwa kufikia mwishoni mwa mwezi.

Wametangaza mgomo kwa muda usiojulikana baada ya mazungumzo kukwama na wamesisitiza kwamba mgomo utaendelea hadi serikali itakapoweka kiwango kipya cha chini cha mshahara wa wafanyakazi.

Forum

XS
SM
MD
LG