Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 16, 2024 Local time: 16:32

Washukiwa watatu wa ugaidi waliokamatwa Brussels waachiwa huru


Polisi wanalichunguza eneo ambalo mshukiwa wa ugaidi Mohammed Abrini alikamatwa mjini Brussels.
Polisi wanalichunguza eneo ambalo mshukiwa wa ugaidi Mohammed Abrini alikamatwa mjini Brussels.

Waendesha mashitaka wa Ubelgiji wanasema kuwa wamewaachia huru watu watatu waliokuwa wanahojiwa kutokana na mashambulizi ya Novemba 13 mjini Paris, ambapo watu 130 waliuwawa.

Ofisi ya mwendesha mashitaka imesema hakuna yeyote aliyefunguliwa mashitaka. Wote hao walikamatwa Jumanne wakati wa msako wa polisi kwenye eneo la Uccle mjini Brussels wakati mamlaka zikiendelea kutafuta washukiwa wa mashambulizi ya Paris na yale ya Brussels kwenye uwanja wa ndege na kituo cha treni ya Machi 22 ambapo watu 32 walikufa.

Mamlaka ya Brussels imelaumiwa kwa kuzembea katika kuwatafuta washukiwa wa mashambulizi hayo.

XS
SM
MD
LG