Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 21:41

Wadhibiti wawili wa vyombo vya habari nchini Guinea wahukumiwa kifungo cha miezi minane jela


Kiongozi wa kijeshi wa Guinea Kanali Mamadi Doumbouya
Kiongozi wa kijeshi wa Guinea Kanali Mamadi Doumbouya

Wadhibiti wawili wa vyombo vya habari nchini Guinea Alhamisi walihukumiwa kifungo cha miezi minane jela baada ya kudai kwamba viongozi wa vyombo vya habari maarufu walikuwa wanapewa hongo na utawala wa kijeshi, wakili wao amesema.

Hukumu hiyo inafuatia ukandamizaji wa miezi kadhaa unaofanywa na serikali ya kijeshi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini kote, ambapo radio nne binafsi na vituo viwili vya televisheni binafsi vilipigwa marufuku mwezi Mei.

Djene Diaby na Tawel Camara, wawili kati ya makamishna 13 wa mdhibiti wa vyombo vya habari HAC, walitozwa pia faini ya dola 116 kila mmoja, wakili Kemoko Malick Diakite aliwambia waandishi wa habari.

Aliongeza kwamba ana nia ya kukataa rufa.

Wakati wa kesi hiyo, mwendesha mashtaka Mohamed Bangoura alikuwa amependekeza kifungo cha mwaka mmoja, akitaja kwamba “vitendo vibaya sana” vilifanywa na makamishna hao.

Mmoja wa mawakili wa utetezi, Bakary Millimouno, aliiomba mahakama iwahurumie wateja wake, akieleza kuwa ni mara ya kwanza wanatenda uhalifu.”

Forum

XS
SM
MD
LG