Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Februari 04, 2023 Local time: 04:51

Wademocratic wanaendelea na mchakato wa mashtaka dhidi ya Trump


Rais wa zamani Marekani, Donald Trump

Waendesha mashtaka wa-Democratic walishtaki maneno na vitendo vya Trump kabla ya shambulizi yalipelekea wafuasi wake kushambulia jengo la bunge wengine wakiwa na silaha wakijaribu kuzuia utaratibu wa uthibitisho wa ushindi wa uchaguzi kwa M-Democratic Joe Biden dhidi ya Trump

Mameneja kutoka chama cha Democratic wanaoshughulikia suala la kufunguliwa mashtaka, pamoja na mawakili wa Donald Trump, Jumanne wameelezea hoja zao katika mukhtasari tofauti kabla ya kupelekwa mbele ya baraza la seneti ili kusikiliza kesi ya Rais wa zamani Marekani Donald Trump wiki ijayo juu ya mashtaka ya kuchochea vurugu kwenye jengo la bunge la Marekani hapo Januari 6.

Waendesha mashtaka wa-Democratic walishtaki kwamba maneno na vitendo vya Trump kabla ya kufanyika shambulizi hilo yalipelekea wafuasi wake kushambulia jengo la bunge wengine wakiwa na silaha wakijaribu kuzuia utaratibu wa uthibitisho wa ushindi wa uchaguzi kwa M-Democratic Joe Biden dhidi ya Trump.

Vurugu hizo zilisababisha vifo vya watu watano akiwemo ofisa polisi wa bunge na darzeni nyingine ya watu walijeruhiwa.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG