Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Julai 27, 2024 Local time: 04:09

Wadau na wanasiasa wakosoa mpango wa serikali ya Tanzania kwa vijana na wanawake katika kilimo


Vijana wakimshangilia rais wa Tanzania Samia Suluhu wakati wa kutangaza mpango wa serikali ya Tanzania unaolenga vijana na wanawake katika kuwaendeleza kwenye kilimo na kuwapatia mashamba makubwa ya pamoja .
Vijana wakimshangilia rais wa Tanzania Samia Suluhu wakati wa kutangaza mpango wa serikali ya Tanzania unaolenga vijana na wanawake katika kuwaendeleza kwenye kilimo na kuwapatia mashamba makubwa ya pamoja .

Wadau wa kilimo, wasomi na wanasiaasa wameukosoa mpango wa serikali ya Tanzania uliolenga vijana na wanawake katika kuwaendeleza kwenye kilimo na kuwapatia mashamba makubwa ya pamoja.

Inatarajiwa watalima mara baada ya kukamilisha mafunzo huku wakitaka kutungwa sheria itakayoweza kusimamia shughuli za kilimo nchini humo.

Wadau wa kilimo, wasomi na wanasiasa wameukosoa mpango wa serikali ya Tanzania uliolenga vijana na wanawake katika kuwaendeleza kwenye kilimo na kuwapatia mashamba makubwa ya pamoja watakayo weza kulima mara baada ya kukamilisha mafunzo huku wakitaka kutungwa sheria itakayo weza kusimamia shughuli za kilimo nchini humo.

Vijana 813 pamoja na wanawake watapatiwa ardhi mara baada ya kupatiwa mafunzo kwa miezi minne yanayohusu kilimo kwa awamu ya kwanza kupitia mradi wa jenga kesho nzuri BBT ulio chini ya Wizara ya Kilimo ambao umezinduliwa na Rais Samia Suluhu jijini Dodoma wenye lengo la kupunguza tatizo la ajira kwa vijana na kuzalisha chakula cha kutosha kitakacho tumika ndani na nje ya nchi.

Baadhi ya wadau wa kilimo wakitilia mashaka utaratibu uliotumika kuwapata vijana hao huku wakisisitiza serikali kuwatumia vijana wanao kujishughulisha na Kilimo toka awali na sio kuwachukua vijana walio maliza chuo ambao kwa muda mwingi wameutumia katika masomo kuliko kwenye Kilimo kama anavyosema Ismail Masudi mmoja wa wadau wa Kilimo kutoka mjini Morogoro anasema "Mimi nafikiria kwamba kuna watu ambao wana uwezo wa kulima ambao wamelima tangu wadogo mpaka sasa kilimo ni kazi yao hao ndio tuwape nguvu halafu vijana wataajiriwa ili kilimo kiwe na tija kwa sababu ukweli ni kwamba wakulima wetu walio wengi wazuri wanalima kilimo cha kizamani".

Maendeleo katika sekta ya kilimo ni muhimu hasa katika kukuza uchumi wa taifa na kuleta msukumo kwenye ukuaji wa sekta ya viwanda na kuzalisha chakula cha kutosha ili kuhakikisha uwepo wa usalama wa chakula na lishe kwa wananchi wakati wote pamoja na kutoa ajira ambapo sekta hiyo imeajiri asilimia 65 ya Watanzania.

Mtutura Abdallah ambaye ni waziri kivuli wa kilimo maendeleo ya mifugo na uvuvi katika serikali kivuli ya ACT wazalendo amesema vijana waliochukuliwa wengi wao wamekwenda kwenye kilimo kwa sababu wamekosa ajira suala ambalo litachangia kudorora kwa mradi huo hivyo ameitaka serikali kuweka sheria ambayo itaweza kuwabana ili kilimo kiweze kuwa na mvuto kwa watu wengi "lakini wangewachukua wale wa vijijini ambao wameishi kwenye kilimo katika maisha magumu sana na wangefanya mazuri zaidi ambayo yangeweza kuwavutia hao wasomi, katika kilimo. kama umakini hauta kuwepo katika haya tulio yazungumzia uwepo wa sheria ya kilimo kwa kweli mafanikio ya mradi huu yatakuwa ni magumu" aliongeza.

Hata hivyo Dkt Ananilea Nkya amesema suala hilo ni zuri licha ya serikali ya Tanzania imekuwa ikifanya mambo mazuri mengi na kuishia njiani huku akionyesha wasiwasi wake kwenye gharama kubwa itakayo tumika ya kuwafundisha vijana ambao hawajawahi kuwa katika ukulima "Lakini kutakuwa na gharama kubwa ya kuweza kuwaelekeza vijana ambao hawaja kuwa wakulima kwenda kuwa wakulima,lakini kama ni mtu amekwenda kwa sababu ni ajira na pana kitu atapewa baadaye hiyo ndio itakuwa hasara kubwa ya taifa kwa sababu tumeiona nchi yetu ikibuni vitu ambavyo sio endelevu" aliongeza,

Rais Samia akihutubia katika uzinduzi wa mashamba hayo amesema hata vumilia pale atakapotoa fedha za wavuja jasho ziende kwenye matumizi ya kilimo na pesa hizo zikachezewa, na kusisitiza kila shilingi itakayowekwa kwenye kilimo iende ikazalishe mara mbili zaidi.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Amri Ramadhani Sauti ya Amerika Dar es Salaam.

XS
SM
MD
LG