Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 06, 2023 Local time: 06:35

Wabunge wa DRC wakosolewa kwa kulipwa mishahara ya juu sana


Spika wa Bunge la DRC, Christophe Mboso, Februari 3, 2021. Picha ya AFP
Spika wa Bunge la DRC, Christophe Mboso, Februari 3, 2021. Picha ya AFP

Madai ya kiongozi wa upinzani wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo kwamba wabunge katika nchi hiyo wanalipwa hadi dola 21,000 kwa mwezi yamezua hasira Jumatano katika taifa hilo, ambalo ni mojawapo ya nchi maskazini zaidi duniani.

Kupata taarifa sahihi kuhusu kiasi gani wabunge wanapata nchini DRC ni vigumu.

Hata hivyo, Jumanne, kiongozi wa upinzani Martin Fayulu alisema katika taarifa kwamba malipo ya wabunge hao yamefikia hadi dola 21,000 kwa mwezi na ameomba uchunguzi ufanyike juu ya suala hilo.

“Ninaghadhabika sana,” alisema, akionyesha kwamba asilimia 70 ya raia wa Congo wapatao milioni 90 wanaishi na chini ya dola 2 kwa siku.

“Huu ni ufisadi kwa kiwango kikubwa,” aliongeza.

Taarifa hiyo iliibua msururu wa makala katika vyombo vya habari vya Congo Jumatano, pamoja na bunge la taifa lenye wabunge 500 kukanusha rasmi madai hayo.

Mbunge Samuel Mbemba, ambaye anafanya kazi na spika wa bunge hilo, ameiambia AFP kwamba Fayulu alikuwa “anaota” kwa kutoa kauli hiyo.

Hata hivyo, Tresor Kibangula, mchambuzi katika taasisi ya utafiti iitwayo Ebuteli, anakadiria kuwa kiwango hicho cha mshahara wa wabunge ni sahihi.

XS
SM
MD
LG