Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 06, 2024 Local time: 22:26

Wabunge Senegal wameanza kujadili pendekezo la kuahirisha uchaguzi


Wabunge katika bunge la senegal
Wabunge katika bunge la senegal

Rais Macky Sall alitangaza kucheleweshwa kwa uchaguzi saa chache kabla ya kampeni kuanza rasmi

Wabunge wa Senegal siku ya Jumatatu walianza kujadili pendekezo la kuahirisha uchaguzi wa rais ambao awali ulipangwa kufanyika Februari 25, kulingana na mwandishi wa habari wa AFP.

Rais Macky Sall siku ya Jumamosi alitangaza kucheleweshwa kwa uchaguzi saa chache kabla ya kampeni kuanza rasmi na kusababisha mgogoro wa kisiasa. Bunge linachunguza maandishi, yaliyopitishwa siku iliyopita na kamati ya maandalizi ikipendekeza kucheleweshwa kwa miezi sita au hata mwaka hadi Februari 2025, kulingana na maandishi yaliyosambazwa kwenye mkutano.

Wafuasi wa Karim Wade, ambaye jitihada zake za kuwania urais zilikataliwa na Baraza la Katiba waliwasilisha pendekezo hilo. Inasema kuwa lengo la kuahirishwa itakuwa kuepuka ukosefu wa utulivu wa kitaasisi na machafuko makubwa ya kisiasa, na kuhakikisha kuanza upya kwa mchakato wa uchaguzi.

Forum

XS
SM
MD
LG