Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Juni 11, 2023 Local time: 04:39

Wabunge Kenya wajiongezea mishahara


Wabunge nchini Kenya wameidhinisha kwa kauli moja mswaada wa kuwapa nyongeza kubwa ya mshahara

Wabunge nchini Kenya wameidhinisha kwa kauli moja mswaada wa kuwapa nyongeza kubwa ya mshahara, mwezi mmoja tu kabla ya kura ya maoni kuhusu katiba mpya ambayo itafanya iwe ni kinyume cha sheria wao kujipangia mishahara yao.

Kuanzia alhamisi wabunge watalipwa dola 13,500 sawa na shilingi milioni moja nukta moja za kenya kwa mwezi, ikiwa kiwango hicho kimepanda kutoka dola 10,500.

Pato la watu kwa mwaka nchini kenya ni dola 783.

Waziri wa fedha wa Kenya Uhuru Kenyata.
Waziri wa fedha wa Kenya Uhuru Kenyata.

Mwanasiasa mmoja, Adan Duale, waziri mdogo wa mifugo aliunga mkono nyongeza hiyo, akisema hakuna kiwango cha fedha ambacho kitatosha kumlipa fidia mbunge kwa majukumu mazito aliyobeba.

Lakini wakenya wanapinga uamuzi huo. Mkuu wa kundi linalotoa shinikizo la kisiasa ameiambia sauti ya Amerika VOA kuwa kundi lake litawafikisha mahakamani wabunge kwa ajili ya nyongeza hiyo, na kutishia kuchukua hatua kama mahakama itakataa kusikiliza kesi yake.

Kama katiba mpya ikipitishwa, wabunge hawataruhusiwa kujiongezea mishahara yao kiholela. Pia watakatwa kodi kwa malipo ya ziada wanayolipwa.

XS
SM
MD
LG