Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Septemba 16, 2024 Local time: 00:01

Wabunge Ghana wapigana bungeni sababu ya mapendekezo ya kodi ya miamala ya kielektroniki

Alban Bagbin (kati) wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress alichaguliwa kuwa spika wa bunge katika Ikulu ya Ghana mjini Accra, Ghana Januari 7, 2021. (Picha na Nipah Dennis / AFP)
Alban Bagbin (kati) wa chama cha upinzani cha National Democratic Congress alichaguliwa kuwa spika wa bunge katika Ikulu ya Ghana mjini Accra, Ghana Januari 7, 2021. (Picha na Nipah Dennis / AFP)

Mapigano yalizuka katika ukumbi wa bunge la Ghana Jumatatu jioni wakati wabunge walipokuwa wakijadili  mapendekezo ya kodi ya miamala ya kielektroniki ambayo yameligawa bunge kwa wiki kadhaa.

Mapigano yalizuka katika ukumbi wa bunge la Ghana Jumatatu jioni wakati wabunge walipokuwa wakijadili mapendekezo ya kodi ya miamala ya kielektroniki ambayo yameligawa bunge kwa wiki kadhaa.

Ushuru wa asilimia 1.75 wa kieletroniki, ambao utajumuisha ushuru wa malipo ya fedha kwa njia ya simu, umepingwa vikali na upinzani tangu ulipopendekezwa kwa mara ya kwanza mwezi uliopita, na kuzuia kupitishwa kwa bajeti ya kitaifa.

Wabunge walifika mbele ya Naibu Spika Joseph Osei-Owusu kupendekeza ushuru huo kujadiliwa na kupigiwa kura kwa utaratibu wa haraka. Wengine walirushiana ngumi na kugombana huku wengine wakiwazuia wenzao.

Waziri wa Fedha Ken Ofori-Atta anadai kwamba ushuru huo ungepanua wigo wa ushuru na kuleta ongezeko la kiasi cha dola bilioni 1.15)kwa mwaka 2022.

XS
SM
MD
LG