Msemaji wa bunge la Uganda Chris Obore, amesema kwamba maambukizi yalikuwa vigumu kuepukika hasa ikizingatiwa kwamba kanuni za kujizuia na maambukizi nchini Tanzania hazitiliwi maanani sana
Wajumbe hao walikuwa wameutembelea mji wa Arusha kwenye michezo ya bunge la Afrika mashariki ambapo Tanzania ilikuwa mwenyeji wa michezo hiyo,ambako makazi ya bunge hilo yanapatikana.
Obore alikuwa miongoni mwa watu waliohudhuria michezo hiyo mjini Arusha wakati ikichukua wiki mbili.Obore anasema kwamba kabla ya kurejea Uganda, wajumbe hao walifanyiwa vipimo vya covid mara mbili, wakiwa Arusha pamoja na kwenye mpaka wa Malaba kwa kuwa walishuku wamepata maambukizi.
Michezo hiyo iliwajumuisha pamoja wabunge kutoka Kenya,Burundi, uganda. Rwanda na sudan kusini.
Msemaji wa wizara ya afya ya Uganda Emmanuel Ainebyoona amesema kwamba wizara yake inafanya kila juhudi kuhakikisha wabunge hao hawaenezi virusi.