Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Desemba 09, 2023 Local time: 10:35

Waasi 55 wauawa Sudan Kusini


Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akifuatana na maafisa wa serikali yake mjini Juba.
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir akifuatana na maafisa wa serikali yake mjini Juba.

Mamia wamefariki katika mapigano kati ya jeshi la kusini na makundi mbali mbali ya waasi tangu mwezi Januari, wakati Sudan Kusini ilipopiga kura kujitenga kutoka kaskazini.

Maafisa wa Sudan Kusini wanasema jeshi limewaua wapiganaji waasi takriban 55 wakati wa mapambano katika jimbo tete la Jonglei.

Msemaji wa jeshi la kusini, Brigadia Jenerali Malaak Ayuen amesema wanajeshi walipambana na wanamgambo walioongozwa na Gabriel Tanginya ambaye aliongoza kundi la wanamgambo ambao lilikuwa likiiunga mkono Khartoum wakati wa virefu vya wenyewe kwa wenyew kati Sudan kaskazini na kusini.

Afisa katika jimbo la Upper Nile huko Sudan Kusini, Peter Lam Both anasema wanajeshi 34 wa jeshi la kusini na raia 43 walijeruhiwa katika mapigano. Hakuna ripoti kuhusu vifo katika jeshi la kusini.

Mamia wamefariki katika mapigano kati ya jeshi la kusini na makundi mbali mbali ya waasi tangu mwezi Januari, wakati Sudan Kusini ilipopiga kura kujitenga kutoka kaskazini. Viongozi wa kusini wanaishutumu kaskazini kwa kuwaunga mkono waasi wanaotaka kudumaza eneo hilo kabla ya uhuru hapo mwezi Julai.

Tanginya alikubali mwishoni mwa mwaka jana wapiganaji wake waingizwe katika jeshi la kusini. Vyombo vya habari vinasema mapigano ya Jumamosi yalianza baada ya wanamgambo kukataa kuripoti katika mji mkuu wa kusini wa Juba.

Maafisa wa kusini wanasema majenerali watano wa Tanginya waliuawa katika mapambano.

XS
SM
MD
LG