Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 18:17

Waasi washambulia Ikulu ya rais Kabila


Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwasili kwa sherehe za kila mwaka za uhuru wa DRC June 30 2010
Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo akiwasili kwa sherehe za kila mwaka za uhuru wa DRC June 30 2010

Watu saba wameuliwa na mmoja kukamatwa baada ya kushambulia Ikulu ya rais mjini Kinshasa. Rais Kabila hakuwepo nyumbani wakati wa shambulio hilo.

Msemaji wa serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, ambaye pia ni Waziri wa Habari Lambert Mende anasema watu waliokua na bunduki walishambulia ikulu ya rais Joseph Kabila na kusababisha mapambano kuzuka na vikosi vya usalama ambapo watu sita wameuliwa.

Akizungumza na Sauti ya Amerika Bw Mende anasema rais Kabila yuko salama na hajaumia kwani hakuwa nyumbani wakati wa shambulio hilo lililotokea katika eneo la Gombe, katika mji mkuu wa Kinshasa.

Bw Mende anasema kiasi ya watu 50 walishambulia nyumba ya rais wakiwa na silaha nzito nzito. Anasema walinzi wa rais waliwasimamisha washambulizi hao kwenye kituo cha ukaguzi na kuwauwa saba kati yao na kuwakamata wengine. Anasema mlinzi mmoja alijeruhiwa vibaya na mapigano yalidumu muda wa dakika 20.

XS
SM
MD
LG