Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Agosti 15, 2022 Local time: 22:24

Waasi waendelea na mauaji Cameroon, HRW yasema


Magari yaliochomwa wakati wa ghasia kati ya vikosi vya serikali na waasi wanatumia lugha ya kizungu kwenye picha ya maktaba

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch limesema Jumatatu kwamba waasi wanaotumia lugha ya kiingereza nchini Cameroon wameua takriba watu 7 pamoja na kuteka nyara watu kadhaa tangu mwanzoni mwa mwaka huu.

Ghasia zimekuwa zikishuhudiwa kaskazini magharibi na kusini magharibi mwa Cameroon kwa karibu miaka mitano wakati serikali ikikabiliana na waasi wanaotumia lugha ya kiingereza wanaotaka kujitenga na wale wanaotumia lugha ya kifaransa, na ambao ni wengi nchini humo.

Waasi hao wamekuwa wakilenga shule pamoja na kushambulia angalau chuo kimoja kikuu. Ripoti ya Human Rights Watch ni kutokana na mahojiano kutoka kwa watu walioathiriwa, mashuhuda, rekodi za kimatibabu pamoja na ushahidi wa kujionea.

Tangu mwaka wa 2017, eneo linalotumia lugha ya kiingereza limedai kutengwa na kwa hivyo kuitisha uhuru wao wa eneo wanaloita Ambazonia. Rais wa Cameroon Paul Biya mwenye umri wa miaka 89 ameongoza taifahilo kwa karibu miaka40, wakati akiamuru misako mikali dhidi ya waasi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG