Sherehe ya kusaini mkataba huo imehudhuriwa na zaidi ya makundi 30 ya waasi , baada ya mazungumzo ya miezi kadhaa mjini Doha, Qatar.
Maelezo zaidi hayajabainisha kuhusu namna mkataba huo utakavyotekelezwa na kufuatiliwa ili kuhakikisha kwamba unaheshimiwa.
Serikali ya mpito, inayoongozwa na Mahamat Idriss Deby, ambaye aliingia madarakani mwaka uliopita baada ya babake, Idirs Deby kuuawa akiwa vitani kupigana na kundi la FACT, imesema kwamba huenda uchaguzi mkuu ukaandaliwa mwaka ujao.
Serikali hiyo ilikuwa imeahidi kuhakikisha kwamba utawala wa kidemokrasia unarejea nchini humo ndani ya kipindi cha miezi 18, lakini hakuna dalili zinaonekana za kutekelezwa ahadi hiyo.