Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 13, 2024 Local time: 05:26

Waasi waliojitenga wadai shambulio la kombora la Jeshi la Ukraine lauwa watu 16.


Mwanamke akitembea mbele ya jengo lililoharibiwa wakati wa mzozo kati ya Ukraine na Rashia katika mji wa Volnovakha unaodhibitiwa na waasi waliojitenga katika jimbo la Donetsk. Machi 11, 2022, picha ya Reuters.
Mwanamke akitembea mbele ya jengo lililoharibiwa wakati wa mzozo kati ya Ukraine na Rashia katika mji wa Volnovakha unaodhibitiwa na waasi waliojitenga katika jimbo la Donetsk. Machi 11, 2022, picha ya Reuters.

Waasi wanaotaka kujitenga wanaoungwa mkono na Rashia mashariki mwa Ukraine wamesema leo Jumatatu kwamba shambulio la wanajeshi wa Ukraine kwenye ngome ya waasi hao katika mji mkuu Donesk limeua watu 16.

Maafisa wa kundi hilo la waasi wamesema mabaki ya kombora hilo la Jeshi la Ukraine aina ya Tochka ambalo lilirushwa na kuanguka katikati ya mji wa Donesk, limesababisha vifo vya Zaidi ya darzeni ya watu na kujeruhi wengine wengi.

Wizara ya afya ya jimbo hilo lililojitenga na Ukraine imesema katika taarifa “ Vifo 16 vimerekodiwa na kuongeza kuwa watu wengine 23 walijeruhiwa”.

Vituo vya matangazo vya eneo hilo lililojitenga vimesambaza picha na video baada ya shambulio hilo, zikionyesha magari yaliyoungua, miili iliyojaa barabarani, na uharibifu wa nje ya maduka.

Shirika la habari la AFP limesema haliwezi kuthibitisha idadi ya vifo iliyotangazwa na maafisa wa eneo hilo lililojitenga, ambalo linadhibitiwa na waasi wanaoungwa mkono na Moscow tangu mwaka wa 2014.

XS
SM
MD
LG