Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Julai 23, 2024 Local time: 14:17

Waasi wakamata visima vya mafuta Libya


Afisa wa usalama wa Libya, anasema wanamgambo wa Kislamu wamechukua udhibiti wa visima viwili vya mafuta kabla ya mazungumzo zaidi ya amani ya Umoja wa Mataifa.

Afisa huyo amesema waasi wameshikilia visima vya Bahi, na Mabrouk, baada ya vikosi vya usalama vya Libya, vilivokuwa na jukumu la kuvilinda kuondoka.

Viwanda vya mafuta vimekuwa ni thamani inayozusha mapigano nchini Libya, baina ya Waislamu wenye msimamo mkali ambao wanashikilia mji mkuu na ambao walivurumushwa kuondoka upande wa mashariki mwa nchi.

Libya imekumbwa na ghasia na machafuko ya kisiasa toka kiongozi wa muda mrefu Moammar Gadhafi, alipotolewa madarakani na kuuwawa mwaka 2011.

Umoja wa mataifa umejitahidi kuleta hali ya utulivu na amani. Mazungumzo ya amani yataanza wiki hii nchini Morocco.

XS
SM
MD
LG