Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Januari 29, 2023 Local time: 09:57

Waasi wafanya mauaji Cameroon


Gari lililochomwa wakati wa ghasia magharibi mwa Cameroon kwenye picha ya awali

Waasi wanaotaka kujitenga nchini Cameroon wameua wanajeshi 15 na raia kadhaa katika mashambulizi mawili ya bomu mwezi huu, serikali imesema Jumatatu, ikiwa awamu nyingine ya mzozo uliodumu karibu miaka mitano na kusababisha vifo vya zaidi ya watu elfu 3.

Waasi wanataka kuunda jimbo huru liitwalo Ambazonia magharibi mwa Cameroon. Walianza kupambana na jeshi mwaka wa 2017 baada ya maandamano ya kutaka watu wachache wanaozungumza Kingereza wawakilishwe ipasavyo katika taifa hilo lenye idadi kubwa ya watu wanaozungumza Kifaransa, kuzimwa kimabavu.

Shambulio la kwanza la mwezi huu lilifanyika tarehe 12 Septemba huko Kumbo, mji ulioko jimbo la kaskazini magharibi, wakati msafara wa kijeshi ukishambuliwa na kilipuzi.

Tarehe 16 Septemba, msafara mwengine katika kijiji cha Bamessing ulishambuliwa kwa vilipuzi, na roketi kabla ya kumiminiwa risasi.

Kutumia zaidi silaha za kisasa ni mabadiliko katika mapigano, wizara ya ulinzi imesema katika taarifa, na kudai kuwa wanamgambo hao wamekuwa wakipata vifaa vyao kutoka makundi yenye itakadi kali ya kidini nje ya Cameroon.

Makundi yenye silaha hayakuweza kupatikana ili kutoa maelezo.

Eneo la magharibi mwa Cameroon linapakana na Nigeria, ambayo ni ngome ya makundi ya wanamgambo yanayofanya mashambulizi mabaya kama Boko Haram na makundi mengine ya majambazi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG