Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 04:35

Waasi wa M23 wakionya kikosi kipya cha Umoja wa Mataifa


Waasi wa M23 wakiwa karibu na mji wa Bunagana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Waasi wa M23 wakiwa karibu na mji wa Bunagana, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Waasi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo-DRC wanasema wanajitayarisha kupambana na kikosi kipya cha Umoja wa mataifa kinachotarajiwa kuwasili huko katika muda wa miezi kadhaa ijayo.

Ofisa wa kundi la waasi la M23, Stanislas Baleke alisema Jumanne kwamba kundi lake lipo katika tahadhari na tayari kwa mapambano.

Kitisho hicho kimetolewa wakati mazungumzo ya amani yanaonekana kukwama kati ya waasi na serikali ya Congo.

Wapiganaji wa kundi la M23 waliteka mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini wa Goma mwishoni mwa mwaka jana na waliushikilia mji huo kwa wiki mbili kabla ya kuondoka.

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeidhinisha kikosi maalumu kwa ajili ya mashariki mwa Congo ambacho kitakuwa na uwezo wa kuyasaka na kushambulia makundi yenye silaha pamoja na kuwalinda raia.

Wakosoaji hata hivyo, wanasema kikosi hicho kinachotarajiwa kuwasili mwezi Julai, huwenda kisitoshe kuleta uthabiti huko mashariki mwa Congo.
XS
SM
MD
LG