Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Aprili 18, 2024 Local time: 03:29

Waasi wa Al-Shabab wadai kumuua Waziri wa Somalia


Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia, Abdi Shakur Sheikh Hassan (katikati) akisindikizwa na wanajeshi mjini Mogadishu.
Waziri wa mambo ya ndani wa Somalia, Abdi Shakur Sheikh Hassan (katikati) akisindikizwa na wanajeshi mjini Mogadishu.

Waasi wa Al-Shagab wada kuhusika na bomu la kujitoa mhanga mjini Mogadishu

Waasi wa kundi la Al-Shabab nchini Somalia wamedai kuhusika na shambulizi la bomu la kujitoa mhanga jana Ijumaa ambalo limesababisha kifo cha waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo.

Afisa mmoja amesema Abdi Shakur Sheikh Hassan aliuawa nyumbani kwake mjini Mogadishu wakati akikutana na washirika wake. Watu kadhaa walijeruhiwa.

Maafisa usalama na shahidi mmoja wamesema mwanamke ambaye anaaminika ni jamaa wa Hassan alijilipua mwenyewe ndani ya nyumba.

Waziri Mkuu Mohammed Abdullah Mohammed ameiambia Idhaa ya Kisomali ya Sauti ya Amerika kuwa shambulizi hilo lilikuwa ni la kinyama na si uislamu.

Al-Shabab imekuwa ikitumia mashambulizi ya kujitoa mhanga ili kupata udhibiti wa Mogadishu na sehemu kubwa za katikati na kusini mwa Somalia kwa takriban miaka mitatu.

Hata hivyo, majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika yamechukua tena sehemu za Mogadishu katika mashambulizi ambayo yalianza mwezi Februari.

Al-Shabab inajaribu kuiangusha serikali ya Somalia inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na kutaka kuunda serikali ya kiislamu.

XS
SM
MD
LG