Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Juni 19, 2024 Local time: 00:30

Waangalizi wa uchaguzi DRC wakosoa uchaguzi


Askari polisi wakiwa wamezingira msafara wa Etienne Tshisekedi Kinshasa Novemba 26, 2011
Askari polisi wakiwa wamezingira msafara wa Etienne Tshisekedi Kinshasa Novemba 26, 2011

Taasisi ya Carter Center yasema uchaguzi wa DRC ulisimamiwa vibaya

Timu ya kimataifa ya wafuatiliaji uchaguzi imesema matokeo ya uchaguzi wa urais uliofanywa mwezi Jana katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo yalisimamiwa vibaya na hayaaminiki. Taasisi ya Carter yenye makao yake nchini marekani inasema uchaguzi huo ambao ulimpa ushindi rais Joseph Kabila kuendelea kuongoza taifa hilo, uligubikwa na kasoro chungu nzima hususan kwenye swala la kuhesabu kura. Katika taarifa iliyotolewa Jumamosi jioni taasisi ya Carter inasema kuna ushahidi kuwa matokeo kutoka takriban vituo elfu 2 vya kupigia kura katika mji mkuu Kinshasa yalipotea. Taasisi hiyo inaongeza kuwa vituo vingi vya kupigia kura kote nchini DRC vilithibitisha kuwa wapiga kura walijitokeza asili mia 99 hadi mia moja na kura karibu zote zikimuunga mkono rais Kabila. Tume ya uchaguzi ya Congo ilitangaza Ijumaa kuwa bwana Kabila ameibuka mshindi wa uchaguzi huo wa Novemba 29. Lakini mpizani wake mkuu Etienne Tshisekedi amepinga matokeo hayo na kujitangaza kuwa rais wa DRC. Lakini mwandishi wa sauti ya Amerika mjini Kinshasa Saleh Mwanamilongo anasema maafisa wa taasisi hiyo ya Carter wamewathibitisghia waandishi habari kuwa japo kulikuwa na kasoro katika hesabu ya kura, rais Kabila bado anaongoza kwa wingi wa kura.

XS
SM
MD
LG