Ethiopia imesema vikosi vyake vya usalama vimewauwa waasi 15 na kuwakamata waandishi wa habari wawili wa Sweden mashariki mwa nchi hiyo.
Msemaji wa serikali Shimeles Kamal alisema jumatatu kwamba vikosi vya usalama viliwauwa waasi kutoka kundi la ogaden national liberation front na kuwakamata waandishi hao
wakati wa mapigano alhamisi iliyopita katika eneo la Somalia.
Eneo hilo linalojulikana kama ogaden linapakana na Somalia.
Kamal alisema waandishi wa habari Johan Person na Martin Schibbye walikuwa wanasafiri na waasi wakati wa mapigano hayo na wametibiwa majeraha madogo.
Waziri wa habari Bereket Simon ameiambia sauti ya Smerika kwamba waandishi hao wawili walijaribu kuingia Ethiopia kutokea Somalia na walijeruhiwa na sisasi.