Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Julai 11, 2025 Local time: 08:11

Waandishi wa habari 14 Malawi wanyang’anywa simu na kompyuta


Greyson Chapita, mfanyakazi wa zamani wa MBC, anasema polisi hawakupata chochote walipopekua simu na kompyuta yake ndogo. Picha kwa hisani ya Greysson Chapita.
Greyson Chapita, mfanyakazi wa zamani wa MBC, anasema polisi hawakupata chochote walipopekua simu na kompyuta yake ndogo. Picha kwa hisani ya Greysson Chapita.

Polisi nchini Malawi wamewanyang’anya simu za mkono na kompyuta ndogo waandishi wa habari 14 wa shirika la utangazaji linalomilikiwa na serikali au MBC, waliokuwa wakishukiwa kufungua akaunti bandia kwa jina la shirika hilo ambapo walidaiwa kubandika habari za kuipinga serikali.

Makundi ya kutetea uhuru wa vyombo vya habari yanailaumu polisi kwa kuingilia faragha ya waandishi hao.

Msemaji wa idara ya polisi Malawi Peter Kalaya, ameiambia Sauti ya Amerika kuwa uchunguzi huo unatokana na malalamiko kutoka wakuu wa Shirika la Utangazaji la Malawi.

“Katika mchakato wa uchunguzi huo, tulipata hati ya upekuzi kutoka mahakamani ambayo tumeitumia kunyang’anya vifaa vya kielekroniki kutoka kwa washukiwa. Vifaa hivyo vinajumuisha simu na kompyuta ndogo” alisema Kalaya.

Kalaya alikataa kutaja idadi kamili ya watu wanaochunguzwa na jinsi walivyoweza kuwatambua kwa tuhuma za kujihusisha na uhalifu mitandaoni,

Hata hivyo, ripoti za vyombo vya habari vya nchi hiyo zinasema kuwa waandishi hao 14 wanaohusika na MBC inajumuisha baadhi ya waliokuwa wameacha kazi kutoka shirika hilo, waliweza kufanya utafiti wa vifaa vyao.

Meneja wa uhusiano wa jamii wa MBC, Chisomo Mwamadi amekataa kuzungumzia uchunguzi huo, akisema shirika hilo la utangazaji limekabidhi kila kitu mikononi mwa polisi.

Forum

XS
SM
MD
LG