Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Desemba 08, 2023 Local time: 03:09

Waandishi Burundi wapinga muswada unaoingilia kazi zao


Waandishi wa habari Burundi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari
Waandishi wa habari Burundi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya uhuru wa vyombo vya habari
Waandishi wa habari nchini Burundi wanapinga muswada mpya ambao wanasema utaingilia uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Bunge la Burundi wiki iliyopita lilipitisha mswada mpya wa vyombo vya habari ambao utawalazimisha waandishi wa habari kuweka wazi vyanzo vya upatikanaji habari zao na marufuku kwa vyombo vya habari kuripoti juu ya masuala yanayoonekana kuwa tete ikiwemo usalama wa umma, ulinzi na uchumi.

Vyombo vya habari ambavyo vitakiuka mipaka hiyo vitakabiliwa na faini ya maelfu ya dola. Bob Rugurika mhariri mkuu katika Radio Puplique Africaine-RPA nchini Burundi, anasema vizuizi hivi havikubaliki.“ kuna vizuizi vingi sana. Sheria inatuzuia sisi kufanya kazi kwenye habari zinazohusu usalama, uchumi na fedha.”

Makundi ya haki za binadamu ikiwemo Committee to Protect Journalists na Amnesty International wanamsihi Rais Pierre Nkurunzinza kukataa sheria mpya, ambapo wanasema inaingilia uhuru wa vyombo vya habari.

Mswada huo ulipitishwa kwa wingi wa kura kutoka wote bunge na baraza la seneti, ambalo limekuwa chini ya udhibiti kamili wa chama tawala tangu upinzani ulipogomea uchaguzi uliopita mwaka 2010.

Wabunge wanasema mswaada huo utawalinda raia na viongozi nchini humo.
Mkurugenzi wa RPA ambaye anaunga mkono upinzani wa zamani anaanza kukata rufaa akiisihi jumuiya ya kimataifa kuweka shinikizo zaidi kwa serikali.

Rugurika anasema wanajaribu kuiangazia dunia. “ mkurugenzi alipeleka barua ya kukata rufaa kwa maseneta wa Marekani na wanasiasa kwa sababu hao ni marafiki wa serikali yetu. Wanaweza kutusaidia sisi kuifanya serikali ifahamu kwamba wanaongoza kwa kufuata njia potofu”.

Serikali ya Burundi karibuni imekuwa na historia ya kuwakamata waandishi wa habari. Rugarika mwenyewe ameshakamatwa mara kadhaa na polisi zaidi ya miaka michache iliyopita. Mwaka 2011 alihojiwa kwa saa 10 baada ya kurusha hewani mahojiano ambayo yaliwahusisha polisi nchini humo katika mauaji ya watu 40.

Mwezi machi maafisa wa polisi walimuachia Hassan Ruvakuki, mwandishi wa habari ambaye alikamatwa mwaka 2011 kwa mashtaka ya ugaidi baada ya kukutana na waasi nchini Tanzania. Anasema alikuwa anafanya kazi yake wakati huo na mashtaka yalipunguzwa wakati wa rufaa yake.
XS
SM
MD
LG