Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Mei 23, 2024 Local time: 02:47

Waandishi 26 washinikiza mkurugenzi wa Sauti ya Amerika ajiuzulu


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Michael Pompeo akizungumza na Mkurugenzi wa VOA Robert Reilly makao makuu ya VOA, Washington, Jan. 11, 2021.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Michael Pompeo akizungumza na Mkurugenzi wa VOA Robert Reilly makao makuu ya VOA, Washington, Jan. 11, 2021.

Waandishi wa habari 26 wanashinikiza mkurugenzi wa Sauti ya Amerika ajiuzulu.

Hatua hii ni baada ya mtiririko wa madai ya hatua za ulipizaji kisasi na ukiukaji wa sheria ambazo zimewekwa kulinda uhuru wa waandishi ziliyopelekea kupewa majukumu mengine mmoja wa waandishi waandamizi wa Sauti ya Amerika, VOA.

Taarifa iliyosambazwa Alhamisi inamshutumu mkurugenzi Robert Reilly na naibu mkurugenzi wake Elizabeth Robbins, kwa kuvunja muongozo unaofuatwa na waandishi wa habari wa VOA kwa kumwezesha afisa wa ngazi ya juu wa serikali “fursa ya kuwa huru kuzungumza mubashara katika matangazo yetu” kwa kuandaa matangazo ya moja kwa moja ya Waziri wa Mambo ya Nje Mike Pompeo na baadae kumuondoa mwandishi wa habari wa VOA White House baada ya kujaribu kumhoji waziri anaye maliza muda wake.

Mike Pompeo alipotembelea.VOA
Mike Pompeo alipotembelea.VOA

Mradi wa Kuiwajibisha Serikali (GAP), usiokuwa wa faida unaowatetea wanaotoa taarifa, umeufahamisha uongozi wa Shirika mama la Vyombo vya Habari vya Umma Marekani, USAGM na VOA, pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Maalum, Ofisi ya Mkaguzi Mkuu, Kamati ya Masuala ya Mambo ya Nje na wabunge wengine, kuwa wale waliosaini malalamiko hayo wanachukuliwa kuwa ni watoa taarifa wanaolindwa.

Patsy Widakuswara, aliyejiunga na VOA mwaka 2003, aliambiwa jioni Jumatatu kuwa anapangiwa majukumu mengine, saa kadhaa baada ya mwandishi huyu maarufu alipojaribu kumuuliza Pompeo na baadae Reilly wakati waziri alipokuwa akiondoka katika jengo la makao makuu ya VOA.

Katika hotuba yake, waziri wa mambo ya nje anayemaliza muda wake alimpongeza Michael Pack, mtendaji mkuu, kwa mabadiliko aliyoyatekeleza USAGM chini ya uongozi wake.

Michael Pack
Michael Pack

Pia aliwapongeza kikundi cha waandishi wa habari wa VOA kwa ushujaa wao katika kuripoti maandamano ya kuunga mkono demokrasia huko Hong Kong.

Widakuswara alikuwa miongoni mwa wale waliotunukiwa tuzo ya Burke kwa kuripoti maandamano ya Hong Kong.

Kufuatia hotuba yake, ambayo pia ilieleza “Tofauti ya Umarekani” na kile anachokiona kama ni jukumu la VOA, Pompeo alihojiwa na Reilly, ambaye hakumuuliza maswali yoyote yaliokuwa yamewasilishwa na chumba kikuu cha habari cha USAGM kuhusu matokeo ya karibuni.

Wakati waziri wa mambo ya nje alipokuwa anaondoka makao makuu ya USAGM, Widakuswara alijaribu bila kufanikiwa kumhoji Pompeo na halafu Reilly, alimkemea Widakuswara, akisema huna ruhusa ya kuuliza maswali.

XS
SM
MD
LG