Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 08, 2022 Local time: 05:43

Pompeo amezungumzia umuhimu wa utangazaji na hadhi maalum ya Marekani duniani


Mike Pompeo, waziri wa mambo ya nje Marekani akiwa makao makuu ya VOA

Mike Pompeo alifanya ziara ya kwanza VOA akiangalia nyuma kuhusu masuala kadhaa ya juu ambayo aliyazungumzia katika ziara zake za nje ya nchi  kama mwanadiplomasia wa juu wa Marekani akisema siku zote tumekuwa katika jitihada ya kuwa na umoja. Ingawaje siyo kila mara tunakuwa sahihi katika hilo

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Mike Pompeo alitembelea makao makuu ya Sauti ya Amerika-VOA Jumatatu ambapo alizungumza kuhusu umuhimu wa utangazaji Marekani na hadhi maalum ya Marekani duniani.

“Nawaeleza watu kuhusu hadhi maalum ya Marekani kila ninapoweza, kwasababu ni kweli. Marekani ni nzuri na kubwa – kila mtu anafahamu na kuelewa vyema tulikotokea. Siku zote tumekuwa katika jitihada ya kuwa na umoja. Ingawaje siyo kila mara tunakuwa sahihi katika hilo. Tunahitaji kuwa wanyenyekevu na wastahmilivu kwa yale yaliyopita na kuangalia yale tuliyanayo sasa.”

Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo (L) na mkurugenzi wa VOA Robert Reilly wakiwa Voice of America, January 11,2021
Waziri wa mambo ya nje Mike Pompeo (L) na mkurugenzi wa VOA Robert Reilly wakiwa Voice of America, January 11,2021

Mwanadiplomasia huyo wa cheo cha juu Marekani alizungumza siku chache baada ya wafuasi wa Rais Donald Trump kuvamia jengo la bunge la Marekani. Picha za vurugu kwenye mfano wa demokrasia ya Amerika zilitawala vichwa vya habari kote duniani. Pompeo alishutumu ghasia za wiki iliyopita lakini tangu wakati huo hajatoa maoni yeyote.

Wakati huo huo mtalaamu mmoja ameiambia VOA kuwa alishtushwa kwamba Pompeo hakuzungumzia ghasia hizo na hakuulizwa kuhusu vurugu ambazo zilitokea sio mbali sana na kwenye jengo ambalo alikwenda kuzungumza.

Michael Kimmage wa mfuko wa German Marshall alisema ilishangaza kwamba waziri Pompeo hakutaja matukio yoyote ya wiki iliyopita,ambayo ni makubwa sana na kwa hakika anadhani yako katika kichwa cha kila mtu.

Serikali ya Marekani inaifadhili VOA na vyombo vingine vya utangazaji kutoa habari kwa wasikilizaji na watazamaji kote duniani katika lugha mbali mbali za kigeni.

Mike Pompeo
Mike Pompeo

Waziri Pompeo aliitaka Sauti ya Amerika kuwa sauti ya kipekee. Amesema utangazaji wa kimataifa wa Marekani una mchango mkubwa katika kuhamasisha maadili ya Marekani kote duniani na siyo sehemu ya kuruhusu utawala wa kiimla kupewa uwanja wa kutoa habari.

“Serikali kama zile za China, Iran, na Korea Kaskazini, hazina heshima kwa hadhi ya kibinadamu ulimwenguni, ambapo Amerika ilianzishwa katika misingi hiyo. Tawala hizo zinachukizwa na kila kitu ambacho taifa letu linasimamia. Tunafahamu kwamba zipo serikali zinazohudumia watu. Wanaamini kwamba watu wapo ili kuihudumia serikali. Kazi ya VOA ni muhimu sana. Ndiyo kiini cha uhuru.”

Muda wa Pompeo kuhudumu kama mwanadiplomasia wa juu unatarajiwa kufika hatima yake baadaye mwezi huu. Rais Mteula Joe Biden amemchagua naibu waziri wa zamani wa mambo ya nje Anthony Blinken kuwa waziri ajaye wa mambo ya nje kama akithibitishwa na baraza la Senate Marekani.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG