Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Oktoba 07, 2024 Local time: 23:47

Waandamanaji washinikiza Netanyahu ajiuzulu na mapigano yasitishwe


FILE PHOTO: Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu
FILE PHOTO: Waziri Mkuu wa Israeli Benjamin Netanyahu

Ikiwa ni miezi tisa tangu vita kuanza huko Gaza, waandamanaji wa Israeli waliziba barabara kuu kote nchini humo Jumapili, wakimtaka Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kujiuzulu na kushinikiza sitisho la mapigano  ili kuwarejesha mateka kadhaa wanaoshikiliwa na Hamas.

Maandamano hayo yamekuja huku juhudi za muda mrefu za amani zikipamba moto wiki iliyopita wakati Hamas ilipoachana na dai lake kuu kwa Israeli kuahidi kumaliza vita hivyo. Kikundi cha wanamgambo bado kinataka wapatanishi kuhakikisha sitisho la kudumu la mapigano, wakati Netanyahu ameapai kuendelea na mapigano mpaka Israeli itakapo angamiza uwezo wa kijeshi na utawala wa wanamgambo wa Hamas.

“Makubaliano yoyote yatairuhusu Israel kurejea na kupigana mpaka malengo yake ya kivita yafanikiwe,” Netanyahu alisema katika taarifa yake Jumapili ambayo ilikuwa na uwezekano wa kuongeza wasiwasi kwa Hamas kuhusu pendekezo hilo.

Ndugu na wanao wasikitia mateka wa Israeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Ukanda wa Gaza.
Ndugu na wanao wasikitia mateka wa Israeli wanaoshikiliwa na Hamas huko Ukanda wa Gaza.

“Siku ya Usumbufu” ya Jumapili ilianza saa 12:29 asubuhi , wakati huo huo ambapo wanamgambo wa Hamas waliporusha roketi za kwanza kuelekea Israel Oktoba 7 na kuchochea vita. Waandamanaji waliziba barabara kuu na kukusanyika nje ya makazi ya mawaziri wa serikali.

Karibu na mpaka wa Gaza, waandamanaji wa Israeli walirusha Maputo 1,500 ya rangi nyeusi na njano kuashiria kuuawa na kutekwa kwa raia wenzao.

Hannah Golan alisema alijitokeza kupinga “kutelekezwa kwa jamii zetu kunakofanywa na serikali yetu.” Aliongeza kuwa: “Ikiwa ni miezi tisa leo, katika siku hii yenye nuksi, na bado hakuna yeyote katika serikali yetu anaye wajibika.”

Wanamgambo wa Palestina waliwauwa takriban watu 1,200 katika shambulizi la kushtukiza na kuwachukua mateka wengine 250. Shambulizi la kulipiza kisasi la Israel limeuwa zaidi ya Wapalestina 38,000, kulingana na Wizara ya Afya katika eneo hilo, hesabu yao haitofautishi kati ya wapiganaji na raia.

Forum

XS
SM
MD
LG