Maelfu ya raia wa Yemen waliandamana katika mji mkuu Sanaa na miji mingine kutaka watoto wawili wa kiume wa rais aliyejeruhiwa Ali Abdullah Saleh kuondoka nchini humo.
Bwana Saleh amelazwa katika hospitali ya Saudi Arabia baada ya kupata na majeraha makubwa katika shambulizi la roketi kwenye makazi yake Juni tatu lakini watoto wake wa kiume wamechukua udhibiti wa jeshi na kushikilia uongozi wa baba yao.
Wanaharakati wengi wapinzani walioandamana Jumapili waliimba nyimbo za kutoa mwito kwa watoto wa bwana Saleh na wajumbe wengine walio karibu naye kuondoka nchini Yemen.
Kijana mkubwa Ahmed anaongoza jeshi la ulinzi la kitaifa wakati mdogo wake Khaled anaoongoza idara maalumu ya jeshi
Wanaharakati wapinzani walioandamana Jumapili waliimba nyimbo za kutoa mwito kwa watoto wa bwana Saleh walio karibu naye kuondoka nchini Yemen.