Waandamanaji walibeba bendera ya Brazil na kuimba wimbo wa taifa katika sikukuu ya kibenki.
Wafuasi wa rais anaye ondoka madarakani Jair Bolsonaro, wameshutumu kufanyika udanganyifu katika mifumo ya uchaguzi ambayo imekuwa ikitumika toka mwaka 1996.
Bolsonaro vilevile amekuwa akitoa madai hayo licha ya kutoa uthibitisho wowote.
Wizara ya ulinzi ya Brasil, hata hivyo imetoa ripoti kupinga madai hayo ya uchaguzi kuwa na udanganyifu huku waangalizi wa kimataifa pia wakithibitisha uhalali wa uchaguzi.
Lula pia alikuwa rais wa Brazil kuanzia mwaka 2003 mpaka 2010 na kuondoka madarakani akiwa anakubalika kwa kiwango kikubwa.