Waandamanaji wanopinga serikali nje ya bunge la Pakistan, hawaonyeshi ishara yoyote ya kuondoka,hadi pale waziri mkuu Nawaz Sharif atakapojiuzulu, dai ambalo serikali imekataa kwa misingi ya kuwai kinyume na katiba. Wakati huo, huo jeshi lenye nguvu la Pakistan limeonya pande zote kutatua mzozo wao kupitia majadiliano.
Maelfu ya waandamanaji wanopinga serikali wamekuwa katikati ya mji mkuu wa Pakistan kwa karibu wiki moja, katika juhudi za kumshinikiza waziri mkuu Nawaz sharif kujiuzulu.
Wote serikali na viongozi wa maandamano hayo hawaelekei kurudi nyuma, na hivyo kuongeza hofu ya mapambano baina ya polisi na waandamanaji hao kila kuchao.
Mwanasiasa wa upinzani Imran Khan na kiongozi mashuhuri wa kidini Tahir-ul Qadri, wameaanda maandamano ya umma, ingawa si kwa ushirikiano lakini wanamtaka waziri mkuu Sharif kuachia madaraka.
Maandamano hayo dhidi ya serikali yamelazimisha sehemu kubwa ya mji huo kufungwa na kuvuruga maisha ya kila siku pamoja na shughuli za kibiashara.