Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Aprili 15, 2024 Local time: 09:59

Waandamanaji wafurika Yemen kupinga sheria mpya


Waandamanaji wa Yemen wakiwa katika maandamano ya kupinga sheria mpya
Waandamanaji wa Yemen wakiwa katika maandamano ya kupinga sheria mpya

Sheria hiyo inampa kibali rais wa nchi hiyo kutokamatwa

Maelfu ya watu wa Yemen walikusanyika katika mji mkuu sana’a Jumapili kupinga kupitishwa sheria inayompa kinga ya kushitakiwa Rais Ali Abdulah Saleh .

Bunge la Yemen lilipitisha sheria hiyo jumamosi. Limetoa kinga kamili kwa bwana Saleh kushitakiwa kisheria kwa tuhuma zozote za uhalifu alioufanya wakati wa utawala wake wa miaka 33 kama faida ya kukubali kujizulu.

Sheria hiyo mpya ni sehemu ya mpango uliohamasishwa na nchi jirani za ghuba wenye lengo la kumaliza miezi kadhaa ya ghasia za kisiasa nchini humo.
Mpango huo ulitiwa saini novemba mwaka jana.


Kinga hiyo imepingwa sana na wapenda demokrasia ambao wamekuwa wakiendesha mapinduzi huko Yemen kwa miezi kadhaa sasa.

XS
SM
MD
LG