Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Machi 04, 2024 Local time: 01:05

Waandamanaji wafunga barabara kuu na madaraja Sudan, polisi wawatawanya


Waandamanaji Sudan.
Waandamanaji Sudan.

Waandamanaji wanaounga mkono jeshi waliziba kwa muda barabara kuu na madaraja katika mji mkuu wa Sudan Jumapili kufuatia mvutano unaozidi kuongezeka baina ya majenerali na vuguvugu la wanaounga mkono demokrasia.

Hayo yalitokea siku moja baada ya mjumbe maalumu wa Marekani kwa ajili ya pembe ya Afrika Jeffrey Feltman kukutana na viongozi wa jeshi na kiraia huko Khartoum kutafuta suluhu ya mzozo uliopo.

Ushirikiano mbovu baina ya jeshi na kiraia katika utawala wa serikali hiyo ya sudan unatishia mfumo tete wa kidemokrasia wa nchi hiyo tangu jeshi lilipomtimua kiongozi wa muda mrefu Omar Al Bashir na serikali yake yenye msimamo mkali wa kiislamu April mwaka 2019 takriban miongo mitatu ya utawala wake.

Mzozo wa hivi karibuni unachochewa pia na jaribio la mapinduzi la mwezi uliopita lililoshindwa.

Maafisa wanashutumu watu walio watiifu kwa Bashir kwa kuchukua hatua hiyo. Lakini majenerali wanashutumu wanasiasa wanaotafuta nafasi za madaraka badala ya kusaidia watu kuondokana na taabu za kiuchumi.

Generali Abdel Fattah Burhan kiongozi wa baraza la kitaifa anasema kuvunjwa baraza la mawaziri la wazirimkuu Adbullah Hamdozk kunaweza kutatua mzozo wa kisiasa unaoiendelea. Hata hivyo pendekezo hilo limepingwa na maelfu ya waandamanaji wanaopenda demokrasia walioingia mitaani kwenye mji mkuu Khartoum na kwingineko nchini humo siku ya alhamisi.

Jumamosi dazani za waandamanaji wanaounga mkono jeshi walivamia sehemu ya mapokezi katika shirika la Habari la taifa na kuchoma matairi moto nje ya ofisi hizo.

kitendo hicho kilichelewesha mkutano wa waandishi wa Habari wa wanaharakati wanaopenda demokrasia , hiyo ni kwa mujibu wa mohamed abdel Hamid mkurugenzi wa shirika la Habari la SUNA.

Wakati huo huo katika hali ya vururugu Jumapili, polisi waliwatawanya waandamanaji kwa kutumia gesi ya machozi ili kufungua barabara kuu walizokuwa wameziba.

XS
SM
MD
LG