Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Aprili 26, 2024 Local time: 09:53

Waandamanaji Sudani Kusini wamewashambulia wanahabari


Wakazi wa Sudani Kusini kabla ya kuwashambulia wanahabari
Wakazi wa Sudani Kusini kabla ya kuwashambulia wanahabari

Waandishi wa habari wasiopungua wawili walipigwa Jumanne na waandamanaji wanaounga mkono serikali katika mji mkuu wa Sudan Kusini, Juba. Mwandishi wa habari mmoja wa nchi za magharibi alijeruhiwa vibaya.

Mamia ya watu wakiwemo vijana, wanawake na machifu wa kikabila walilaani uamuzi wa Marekani wa wiki iliyopita wa kuiwekea nchi yao vikwazo vya silaha. Baraza la machifu wa Sudan Kusini waliandaa maandamano na baadhi ya wafuasi wake walipanda malori hadi kwenye mitaa ya Juba wakiwasihi wakazi wa huko kuandamana.

Mashahidi walisema ghasia ambazo zilitokea nje ya uwanja wa jengo la ofisi za Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini-UNMISS karibu na uwanja wa ndege wa kimataifa wa Juba zilihusisha zaidi vijana ambao walionekana kutoa hasira zao kwa mataifa ya kigeni.

Mwandishi mmoja wa habari mwanamke ambaye alishambuliwa alikataa kutaja jina lake lakini aliiambia “Idhaa ya Sudani Kusini ya Sauti ya Amerika” kwamba vijana wenye hasira walimpiga maeneo ya usoni, walijaribu kumfunga Kamba na kumuangusha chini.

XS
SM
MD
LG