Ranil aliteuliwa kuwa rais wa mda wa Sri Lanka baada ya Gotabaya Rajapaska kukimbilia nchi hiyo na kwenda uhamishoni ambapo alitangaza kujiuzulu kufuatia maandamano ya miezi kadhaa.
Maandamano yamekuwa yakiendelea Sri Lanka baada ya uchumi wa nchi hiyo kuanguka.
Kaimu rais Ranil, alitangaza hali ya dharura na kumpa mamlaka makubwa ya kuongoza nchi hiyo licha ya maandamano kuongezeka kutaka ajiuzulu.
Bunge la Sri Lanka linatarajiwa kumchagua rais mpya katika mda wa siku mbili.
Waandamanaji wamesema kwamba tangazo la hali ya dharura halitawazuia kuendelea kutaka kuundwa kwa serikali mpya.
Maandamano hayo yanaingia siku ya 100, huku Zaidi ya watu milioni 22 wakikabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, mafuta na dawa tangu mwishoni mwa mwaka uliopita.