Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 29, 2022 Local time: 23:28

Mali: Waandamanaji wakataa mapendekezo ya wapatanishi, wataka Rais Keita kung’atuka


Mmoja wa waandamanaji nchini Mali.

Maelfu ya waandamanaji Jumatano walijitokeza kwenye barabara za mji mkuu wa Mali, Bamako, katika maandamano mapya kumtaka rais Ibrahim Bounacar Keita kujiuzulu licha ya kuwepo juhudi za kimataifa za kuleta marishiano ili kumaliza mgogoro wa kisiasa nchini humo.

Maandamano yameongozwa na kundi la wanasiasa wa upinzano la

M5-RFP. Maandamano yamekuwa yakifanyika tangu mwezi Juni baada ya uchaguzi wa mitaa ambao unaripotiwa kukumbwa na dosari.

Waandamanaji pia yanapinga ongezeko la visa vya ufisadi serikalini.

Wasiwasi uliongezeka mwezi Julai baada ya polisi kupiga risasi na kuua watu 11.

Viongozi wa kanda hiyo wana wasiwasi kwamba maandamano ya muda mrefu yanaweza kutatiza juhudi za kupambana na makundi ya wanamgambo wa Kiislamu ambayo yanaaminika kutekeleza mashambulizi kutoka Mali.

Serikali ya Mali imeshindwa kuongoza sehemu kubwa ya katikati na kaskazini mwa nchi kutokana na makundi ya wapiganaji.

Rais Keita amekuwa na matumaini kwamba mapendekezo ya wapatanishi yangekubaliwa na wapinzani wake.

Lakini idadi kubwa ya waandamanaji wameinga mjini Bamako, wakipaaza sauti za kutaka Keita kuwasikiliza watu wa taifa hilo na kujiuzulu.

-Imetayarishwa na Kennes Bwire, VOA, Washington DC

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG