Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 15:27

Waandamanaji Bangladesh wapinga utetezi wa Macron juu ya ukosoaji wa Uislam


Maandamano nchini Bangladesh kushinikiza kususia bidhaa za Ufaransa yakilaani kauli ya utetezi iliyotolewa na Rais Emmanuel Macron juu ya ukosoaji wa Uislamin Dhaka, Bangladesh, Oktoba 27, 2020. REUTERS/Stringer
Maandamano nchini Bangladesh kushinikiza kususia bidhaa za Ufaransa yakilaani kauli ya utetezi iliyotolewa na Rais Emmanuel Macron juu ya ukosoaji wa Uislamin Dhaka, Bangladesh, Oktoba 27, 2020. REUTERS/Stringer

Nchini Bangladesh watu wasiopungua 50,000 waliingia kwenye barabara za mji mkuu Dhaka Jumatatu kumpinga Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ambaye ametetea ukosoaji wa Uislamu kama haki ya uhuru wa kuzungumza.

Waandamanaji hao walidai kususiwa kwa bidhaa za Ufaransa na kujaribu kuandamana kwenda kwenye ubalozi wa Ufaransa lakini walizuiliwa na polisi.

Ufaransa ni mshirika muhimu wa kibiashara na mtoaji mkuu wa misaada kwa Bangladesh.

Polisi walikadiria kuwa karibu watu 50,000 walishiriki katika maandamano hayo, lakini waandaaji walisema zaidi ya watu 100,000 walikuwa wamekusanyika kwenye mkutano huo.

Macron alisababisha maandamano katika ulimwengu wa Kiislamu, ikiwa ni pamoja na Bangladesh, wakati aliposema Ufaransa haitawahi kukana haki yake ya kuchora vibonzo.

Maoni yake yalikuja baada ya kuchinjwa kwa mwalimu Samuel Paty mapema Oktoba ambaye alikuwa amewaonyesha wanafunzi katuni ya Mtume Muhammad iliyochapishwa tena na jarida lenye makao yake katika jiji la Paris Charlie Hebdo.

XS
SM
MD
LG