Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Machi 28, 2023 Local time: 21:13

Waandamanaji 7 wauawa katika maandamano ya kupinga utawala wa kijeshi nchini Sudan


Watu wakiimba na kuchoma matairi katika maandamano ya kulaani mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba 2021, mjini Khartoum, Januari 6, 2022. Picha ya AP

Waandamanaji wasiopungua 7 wameuawa Alhamisi nchini Sudan wakati maafisa wa usalama wakijaribu kuzuia mikusanyiko mikubwa ya waandamanaji wanaodai kumalizika kwa utawala wa kijeshi, madaktari wanaounga mkono demokrasia wamesema.

Katika moja ya siku zilizoshuhudia vurugu mbaya zaidi mwaka huu, waandishi wa shirika la habari la AFP wameripoti kwamba maafisa wa usalama walionekana wakiwatawanya maelfu ya waandamanaji kwa kutumia gesi ya kutoa machozi na guruneti bandia, huku baadhi yao wakikaidi amri.

“Hata tukifa, jeshi halitatutawala”, waandamanaji wamesikika wakiimba, wakihimiza kubatilishwa kwa mapinduzi ya kijeshi ya Oktoba yaliyoongozwa na mkuu wa jeshi Abdel Fattah al-Burhan ambayo yalipelekea serikali za kigeni kupunguza misaada, na kuzidisha mzozo wa kiuchumi.

Watano kati ya saba waliuawa kwa kupigwa risasi, wawili walipigwa risasi kifuani, wawili kichwani, na mwingine mgongoni, kamati kuu ya madaktari imesema, na kuongeza idadi ya jumla ya vifo kufikia 110 kutokana na ghasia zinazohusiana na maandamano tangu mwezi Oktoba mwaka jana.

“Tumechoka na utawala wa Burhan, umati wa watu uliimba, huku maandamano na ghasia vikipamba moto katika mji mkuu wa Khartoum na vitongoji vyake, ukiwemo mji pacha wa Omdurman, ng’ambo ya pili ya mto Nile.

Maafisa walifyatua mabomu ya maji ya kuwasha, huku waandamanaji wakichoma moto matairi.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG