Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Aprili 02, 2023 Local time: 15:17

Waandamana Khartoum, Sudan, kupinga uhusiano na Israel


Raia kadhaa wa Sudan waliandamana katika mji mkuu Jumatatu kupinga uhusiano wa kidiplomasia na Israel, baada ya ziara ya wiki iliyopita ya kushangaza ya waziri wa mambo ya nje wa Israel. 

Dazeni ya waandamanaji wa Sudan waliimba “hakuna hali ya kawaida” na Israel, huku wakiwa na mabango yakisema kiongozi wa kijeshi wa Sudan, Abdul Fattah al-Burhan ametenda usaliti.

Maandamanio ya Jumatatu yamefanyika baada ya maafisa wa Sudan na Israel kutangaza kwamba mataifa hayo mawili yanaelekea kuwa na uhusiano wa kawaida.

Tangazo lilitolewa Alhamisi baada ya ziara ya kikazi ya waziri wa mambo ya nje wa Israel, Eli Cohen, ambaye alikutana na maafisa wa Sudan mjini Khartoum.

Akiongea na VOA wakati wa maandamano ya Jumatatu, muandamanaji Mohammed Ali Safi amesema anapinga uhusiano wa namna yoyote wa kawaida na Israel.

Amesema wapo katika wizara ya mambo ya nje kupaza sauti kwamba Khartoum inapaswa kubakia kuwa mji ambao unasema ‘hapana kwa amani, hapana uhusiano wa kawaida, na kutoitambua Israel.

Sera ambayo inafahamika kama “Three Nos” ilianzishwa mwaka 1967 katika mkutano wa jumuiya ya mataifa ya kiarabu, mara baada ya vita vya mashariki ya kati vya 1967 ambapo Israel ilichukua udhibiti wa Jerusalem na ukingo wa magharibi.

Muandamanaji mwingine, Tamadur Omer anasema ameshiriki maandamano kupinga hatua isiyo halali ya uamuzi uliochukuliwa na viongozi wa kijeshi wa Sudan.

Amesema dini yake hairuhusu kuishi kwa amani na watu wa Israel, na ndio maana uamuzi wa serekali hauna maslahi kwa watu wa Sudan.

Amesema kama Muislamu, ninapinga hatua za kuweka uhusiano wa kawaida na desturi. Na kama watu wa Sudan, hatutauza nchi yetu kwa Wayahudi. Anasema uamuzi kama huo unaweza kufanywa na serekali halali na iliyo chaguliwa.

Abdulrahman Khaleel, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Sudan, haja chukulia maandamano hayo kwa usito mkubwa akisema watu wapo huru kuandamana.

“Ni kawaida kwamba sehemu ya Wasudan wanapinga hili. Wana haki ya kutoa maoni yao.”

Mwaka 2020 Umoja wa falme za kiarabu, Bahrain, na Morocco zote zilianzisha uhusiano wa kawaida na Israel ikiwa ni sehemu ya mkataba ulio simamiwa na Marekani. Sudam peke yake ilitangaza mipango ya kuanzisha uhusiano na Israel katika makubaliano yaliyosimamiwa na utawala wa rais wa zamani wa Marekani Donald Trump.

Januari 2021, serekali ya Sudan ilitoa azimio likifungua njia ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel, na baadaye iliidhinishsa mswaada wa kukomesha kuisusia nchi iliyoanzishwa mwaka 1968.

Facebook Forum

XS
SM
MD
LG