Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Novemba 06, 2024 Local time: 09:00

Waachimba madini 500 waokolewa Afrika Kusini


Zaidi wachimba madini 500 ambao walikuwa chini ya adhi kwa takribani siku tatu katika mvutano baina ya vyama pinzani vya wafanyakazi wa Afrika Kusini, walirejeshwa juu Jumatano wamesema polisi.

Baadhi ya wachimba madini 455, ikijumuisha watoa huduma ya kwanza, na walinzi walitolewa mchana baada ya kundi la watu 107 kurejeshwa juu asubuhi, amesema msemaji wa polisi Brenda Muridili.

Wachimbaji hao walishindwa kuondoka ardhini katika mgodi wa Gold One, uliopo Springs, mashariki mwa Johannesburg, baada ya kumalizika zamu ya usiku Jumatatu.

Chama cha wafanyakazi cha NUM moja ya vyama vinavyohusishwa na utawala wa mgodi umesema wafanyakazi wao walishikiliwa mateka na wanachama wa chama cha wafanyakazi cha AMCU.

Hata hivyo AMCU imepinga kuhusika.

Forum

XS
SM
MD
LG