Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Juni 05, 2023 Local time: 02:09

Afrika Kusini yapiga kura leo


Masanduku ya kura yanavyoonekana katika mji wa Cape Town, Afrika kusini kwa ajili ya upigaji kura, Mei 7, 2014
Tume huru ya uchaguzi nchini Africa Kusini-IEC imejiandaa vyema kufanya uchaguzi wa kitaifa na wa majimbo unaofanyika Jumatano, Mei 7.

Ikitajwa kama aina maalum ya kura, wapigaji kura ambao ni wagonjwa, maafisa wa usalama na maafisa wa uchaguzi ambao watakuwa wakifanya kazi siku ya uchaguzi waliruhusiwa kupiga kura mapema kabla ya uchaguzi.

Msemaji wa tume huru ya uchaguzi ya Afrika kusini, Kate Bapela, anasema “Waafrika kusini ambao wamepiga kura ngambo na mbele ya mipaka ya Afrika kusini wameshamaliza kupiga kura na tumefurahi na maendeleo. Tayari kura zilizopigwa zinaletwa nchini kuweza kuhesabiwa na kura zitakazo pigwa siku ya uchaguzi hii leo Mei 7”.

Bi. Bapela anasema hatua zimechukuliwa kuhakikisha kusadikika kwa kura hizo. “Tuko tayari kabisa, kwa sababu tufikapo katika kituo cha matokeo, ni ishara bayana kwamba tuko tayari kuendelea na uchaguzi. Maafisa wetu wametayarishwa, mfumo wa kutowa matokeo uko tayari kuweka matokeo kadri yanavyotokea katika vituo vya upigaji kura kote nchini”.
Baadhi ya wakazi huko Cape Town wakisubiri usafiri wa taxi kuelekea vituo vya kupiga kura
Baadhi ya wakazi huko Cape Town wakisubiri usafiri wa taxi kuelekea vituo vya kupiga kura


Matokeo ya kura kutoka vituo vya uchaguzi kote nchini yatahesabiwa katika makao makuu ya IEC ili kutathmini matokeo ya mwisho ya uchaguzi.

Kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi ya Afrika kusini, IEC inaweza kutangaza matokeo ya uchaguzi katika kipindi cha siku saba baada ya kuhitimishwa kupigwa kura.
Bi Bapela anasema anadhani ifikapo Ijumaa matokeo mengi yatakuwa yamefika na iwapo kila kitu kitakuwa sawa basi lazima tutangaze matokeo mwishoni mwa wiki ijayo. Anasema haya yote yanategemea uwezo wa maafisa wetu kuweza kuweka matokeo na kuhakikisha kila kitu kimefanywa ipasavyo. Anasema maafisa wa tume ya uchaguzi wamepatiwa mafunzo ya kutosha ya kuandaa uchaguzi na kuahidi kufanya uchaguzi uliowazi.

Anasema anatumai watapata si chini ya asilimia 70 ya wapigaji kura na wanataraji kwamaba wa- Afrika kusini watajitokeza kwa idadi kubwa na kutumia fursa hii kadhalika kusheherekea miaka 20 ya demokrasia.

Takwimu za maoni za hivi karibuni zinaonyesha kwamba chama tawala cha Africa National Congress-ANC kitashinda uchaguzi licha ya ushindani mkali kutoka kwa vyama vya upinzani ikiwa ni pamoja na chama cha Democratic Alliance-DA.
XS
SM
MD
LG