Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Machi 29, 2024 Local time: 10:40

Vyombo vikuu vya habari vya Ufaransa vyazuiliwa kutangaza nchini Mali.


Kanali Assimi Goita, kiongozi wa mapinduzi mawili ya kijeshi akiapishwa kama rais wa mpito mjini Bamako, Mali, Juni 7,2021. Picha ya Reuters.
Kanali Assimi Goita, kiongozi wa mapinduzi mawili ya kijeshi akiapishwa kama rais wa mpito mjini Bamako, Mali, Juni 7,2021. Picha ya Reuters.

Utawala wa kijeshi nchini Mali Jumatano usiku uliviamuru vyombo vya habari vya Ufaransa, radio RFI na televisheni ya France 24 kutopeperusha tena matangazo yao nchini humo, ukilalamika kuwa vyombo hivyo vya habari vililishtumu kwa uongo jeshi la Mali kufanya unyanyasaji.

Msemaji wa jeshi, Kanali Abdoulaye Maiga amesema “ Serikali ya Bamako inakanusha kabisa shutma hizi za uongo dhidi ya jeshi jasiri la Mali ( FAMA)”.

Maiga ameongeza kuwa “ Utawala wa kijeshi umeanzisha mchakato wa kusitisha matangazo ya RFI na France 24 hadi itakapotolewa taarifa nyingine.

RFI na France 24 zilikuwa bado zinatangaza Alhamisi asubuhi katika taifa hilo la eneo lenye mgogoro la Sahel.

Hakuna tukio la hivi karibuni ambapo vyombo muhimu vya habari vya kigeni vilikatazwa kupeperusha matangazo.

RFI na France 24 zinatoa taarifa nyingi za habari nchini Mali na zina wasikilizaji wengi.

Utawala wa kijeshi ambao ulichukuwa madaraka Agosti 2020, umesema kulikuwa na madai ya uongo katika ripoti ya wiki hii ambapo RFI ilipeperusha maelezo ya watu wanaodaiwa kuwa waathirika wa unyanyasaji uliofanywa na jeshi la Mali na Mamluki wa kundi la Rashia, Wagner.

XS
SM
MD
LG