Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Juni 22, 2024 Local time: 15:39

Uganda yafungua kiwanda cha kutengeneza vyandarua kupambana na Malaria


Iyandarua vya kuzuia mbu.
Iyandarua vya kuzuia mbu.

Waziri wa Biashara wa Uganda, Amelia Kyambadde, amefungua kiwanda cha kutengeneza vyandarua vya kuzuia mbu ambacho kimegharimu dola za Kimarekani millioni mbili nukta tatu. Kiwanda hicho kitakuwa kikitengeneza vyandarua milioni tatu ambavyo vitakuwa vimenyunyiziwa dawa ya kuua mbu.

Gazeti la Monitor, linalochapishiwa mjini Kampala, limeripoti leo kwamba kiwanda hicho kimejengwa kwa ushirikiano na makampuni mawili, Sino Africa Medical Devices Company Limited na Tiyajin Yorkoor International Company Limited.

Wakati wa uzinduzi huo, Bi Kyambadde alisema pamoja na kuwa na manufaa makubwa kwa sekta ya afya, kiwanda hicho pia kitasaidia kukuza uchumi kwa kutoa ajira. Waziri huyo aliongeza kwamba anatumai kiwanda hicho kitatengeneza vyandarua hivyo kwa kutegemea pamba inayokuzwa nchini Uganda huku akiongeza kwamba nchi hiyo ina mali ghafi ya kutosha.

Naye waziri wa afya Dr Elioda Tumwesgigye, ambaye pia alihudhuria hafla hiyo, alisema serikali itaokoa kiasi kikubwa cha fedha kwa sababu sasa imekoma kununua neti hizo kutoka nchi za nje.

Balozi wa China nchini Uganda, Zhao Yali, alisema nchi yake iko tayari kushirikiana na serikali ya Rais Yoweri Museveni ili kuimarisha maisha ya Waganda.

XS
SM
MD
LG