Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 01:13

Vyama vinavyosimamia soka duniani vyatishia klabu au mchezaji atakayeshiriki Ligi Kuu mpya Ulaya


Mshabiki wa Tottenham Hotspur akishika bango la kupinga Super League nje ya uwanja wa Tottenham Hotspur wakati timu 12 zikipanga kuanzisha Super League.
Mshabiki wa Tottenham Hotspur akishika bango la kupinga Super League nje ya uwanja wa Tottenham Hotspur wakati timu 12 zikipanga kuanzisha Super League.

Vyama vinavyosimamia soka duniani vimetishia kupiga marufuku klabu au mchezaji yeyote atakayeshiriki Ligi Kuu mpya ya Ulaya- Super League kucheza katika mashindano yao, na kuibua uwezekano kwamba baadhi ya nyota wakubwa ulimwenguni wanaweza kupigwa marufuku kuwakilisha nchi zao kwenye Kombe la Dunia la FIFA.

Mistari ya mapambano inachorwa kwa mustakabali wa mpira wa miguu, baada ya vilabu kadhaa vya juu vya Ulaya kusaini kwenye mashindano hayo ya kujitenga, ambayo wakosoaji wanasema yataharibu muundo wa jadi wa mchezo huo. Kwa pande zote mbili, vikosi vyenye nguvu vinajipanga kwa vita ambayo inaweza kuamua mustakabali wa mchezo huo wa ulimwengu.

Vilabu sita kutoka Uingereza - Liverpool, Manchester United, Manchester City, Arsenal, Tottenham Hotspur na Chelsea; tatu kutoka Uhispania - Barcelona, Real Madrid na Atletico Madrid; na tatu kutoka Italia - AC Milan, Inter Milan na Juventus awali walisaini kwenye Ligi hiyo Kuu ya Ulaya ambayo muundo wake ulitangazwa Jumatatu.

Walakini, saa chache tu baada ya tangazo hilo, Manchester City ilithibitisha Jumanne kwamba hawatashiriki tena kwenye mashindano hayo. Iliripotiwa kuwa Chelsea pia ina mpango wa kujitoa.

Waandaaji wa Ligi hiyo Kuu ya Ulaya -Super League wanasema mashindano hayo mapya yangetoa ushindani lakini hayatachukua nafasi ya ligi zilizopo za nyumbani na mashindano ya Ulaya kama vile Ligi ya Mabingwa ya UEFA.

XS
SM
MD
LG