Kampuni ya kutengeneza magari ya Volkswagen imefikia makubaliano na Serikali ya Marekani pamoja na jimbo la California Jumanne dhidi ya shutuma za udanganyifu wa majaribio ya hewa chafu kwenye magari yanayotumia mafuta ya Diesel katika mpango unaotarajiwa kugharimu watengenezaji wa magari hayo dola bilioni moja. .
Chini ya mkataba huo kati ya idara za mahakama ulinzi na mazingira kutoka jimbo la California, kampuni hiyo lazima inunue tena au irekebishe magari 83,000 yaliotengenezwa kuanzia 2009 hadi 2016 yakiwemo yale ya aina ya Porsche na Audi yaliotengenezewa kwenye kiwanda cha Volkswagen. Kampuni ya Volkswagen ingali inakabiliana na mashitaka kutoka kwa watu binafsi.
Jimbo la California lilishitaki kampuni hiyo kwa kukiuka sheria zake za kimazingira.