Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:45

VOA yafanya mahojiano na Obama


Rais Obama akizungumza na mwandishi wa Sauti ya Amerika Andre de Nesnera katika ikulu Washington
Rais Obama akizungumza na mwandishi wa Sauti ya Amerika Andre de Nesnera katika ikulu Washington

Mahojiano na VOA yalifanyika muda mfupi kabla Rais Obama kulihutubia taifa kuhusu upunguzaji wanajeshi Afghanistan

Katika mahojiano maalum na Sauti ya Amerika Rais Barack Obama alielezea kwanini Marekani inaanza kuondoa majeshi kutoka Afghanistan. Anasema hali inabadilika na kwa sababu hiyo ataanza kuondoa majeshi mwezi ujao.

“ Tunachofanya sasa ni kuondoa wanajeshi 10,000 ifikapo mwisho wa mwaka na wanajeshi wa ziada 23,000 ifikapo mwisho wa kipindi kijacho cha majira ya joto”.

Bw. Obama amesema bado kutakuwa na vikosi kadhaa vya Marekani huko Afghanistan . Na aliamua kuondoa majeshi baada ya kushauriana na wakuu wa jeshi na serikali ya Afghanistan.

Rais wa Afghanistan Hamid Karzai katika miezi ya karibuni ameikosoa Marekani na washirika wake wa NATO jinsi wanavyoendesha vita hiyo, hasa kwa vifo vya raia . Lakini rais Obama amesema Bw. Karzai ana malengo sawa ya kimkakati kama ya Marekani, na kwamba marekani inataka serikali ya Afghanistan iliyo huru na salama na ambayo inaweza kuamua inakokwenda.

Rais Obama anakiri kwamba kuna aina fulani ya kuchoshwa na vita hapa Marekani. Rais amesema hakuna shaka hata kidogo kwamba baada ya miaka karibu 10 ya vita huko Afghanistan na idadi ya watu waliopoteza maisha yao na fedha zilizotumika watu wamechoshwa.

XS
SM
MD
LG