Wizara ya ulinzi ya Russia imesema kwamba iliangusha ndege zisizokuwa na rubani 68 zilizorushwa na Ukraine, usiku wa kuamkia leo, ikiwa ni pamoja na 10 zilizopita juu ya mji wa Smolensk.
Makombora mengine yamezuiliwa katika miji ya Bryansk, Crimea, Krasnodar, Tver, Rostov, Kursk na Kaluga.
Hakuna ripoti zaidi za uharibifu au vifo.
Wakati huo huo, mfumo wa ulinzi wa Ukraine umezuia makombora yaliyorushwa na Russia katika mji wa Kyiv, leo Jumanne.
Kiongozi wa kijeshi katika mji wa Kyiv, Serhii Popko, amesema mabaki kutoka kwa makombora yaliyozuiliwa yameangukia ajengo lakini hakuna uharibifu ulitokea.
Forum