Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Aprili 20, 2024 Local time: 18:57

Watu zaidi wajeruhiwa Iraq


Idadi ya raia wanaojeruhiwa inazidi kuongezeka wakati vita vya kuuteka mji unaoshikiliwa na kundi la Islamic State wa Fallujah vinapamba moto.

Jon Egeland wa Baraza la Wakimbizi la Norway anasema “Janga la kibinadamu linaanza kujitokea huko Fallujah. Familia zinajikuta kati kati ya mapigano bila ya kujua wapi pa kwenda kupata hifadhi ya usalama."

Jeshi la Iraq lilianzisha mashambulizi yaliolenga kuukomboa mji huo mwishoni mwa wiki iliyiopita.

Watoto wasiopungua 20,000 wamekwama katika mji huo kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Idara ya Watoto ya Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Idara hiyo imezitaka pande zote kuhakikisha usalama wa watoto hawo ambao wako hatarini kuandikishwa kua wapiganaji.

XS
SM
MD
LG