Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Oktoba 08, 2024 Local time: 00:28

Vita vya Israel- Hamas: Blinken amesema mafanikio yapo katika kuwalinda raia wa Palestina


Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza na waandishi wa habari huko New Delhi, Novemba 10, 2023. Picha na REUTERS
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken akizungumza na waandishi wa habari huko New Delhi, Novemba 10, 2023. Picha na REUTERS

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken alisema, "mafanikio kadhaa yamepatikana katika kuwalinda raia wa Palestina, lakini "mengi zaidi yanahitajika kufanywa" ili kupunguza idadi ya majeruhi na usambazaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo la Gaza lililokumbwa na vita.

"Tumeona maendeleo, tunahitaji kuona zaidi," Blinken aliwaambia waandishi wa habari mjini New Delhi mwishoni mwa ziara ya siku tisa katika nchi nane, ziara ambayo kwa sehemu kubwa ililenga mzozo unaozidi kuwa mbaya huko Mashariki ya Kati.

Israel siku ya Alhamisi ilikubali kusitisha operesheni yake ya kijeshi dhidi ya wanamgambo wa Hamas katika baadhi ya maeneo ya kaskazini mwa Gaza kwa saa nne kila siku, kulingana na maafisa wa White House.

Sitisho la mapigano linalenga kuruhusu kuingia kwa misaada zaidi ya kibinadamu, pamoja na Wapalestina wanaotaka kukimbia maeneo ambayo operesheni ya ardhini ya Israel na mashambulizi makali ya anga.

Siku ya Alhamisi, Israel pia ilifungua njia ya pili kwenye pwani ya Gaza, ambayo inawaruhusu Wapalestina zaidi kukimbia vita, maafisa wa White House walisema. "Kile ambacho Israel ilitangaza jana kitasaidia," Blinken alisema, akiongeza kuwa Marekani pia inajadili "hatua madhubuti" ambazo zitaruhusu utoaji wa mara kwa mara wa misaada ya kibinadamu, pamoja na mafuta kwa ajili ya vituo muhimu, kama vile hospitali na mitambo ya kusafishia maji.

Zaidi ya watu 10,000, karibu asilimia 40 kati ya hayo ni watoto, wameuawa wakati wa mashambulizi makubwa ya Israel huko Gaza katika mwezi mmoja uliopita, kulingana na maafisa wa Palestina. Kwa kweli, idadi hiyo inaweza kuwa kubwa zaidi, kulingana na afisa mkuu wa utawala wa Biden ambaye alitoa ushuhuda Bungeni siku ya Jumatano.

Forum

XS
SM
MD
LG